Breaking News
Loading...
Monday, 9 April 2018

Info Post



Straika wa Tottenham Harry Kane amesema kwamba anajiamini anaweza kumpiku nyota wa Liverpool Mohamed Salah katika mbio za kuwania kiatu cha dhahabu msimu huu.

Kane anawania kumaliza mfungaji bora wa ligi kwa msimu wa tatu mfululizo , mara ya mwisho ni Thierry Henry ndio aliweza kufanya hivyo kuanzia 2003 hadi 2006.

Straika huyo ambaye amefunga mara 24 msimu huu yupo nyuma kwa magoli matano dhidi ya Salah .

Spurs wamebakiza mechi 6 kabla ya ligi kuisha huku Liverpool wakibakiza mechi 5 , na Kane anaamini kwamba anaweza kumpiku Salah.

" Bado naamini naweza. Sikiliza, chochote kitakachotokea bado kuna mechi zimebaki . Natakiwa kufikiria kuhusu kiwango changu, na siwezi kudhibiti anachokifanya Salah."

" Ni wazi kwamba kama Straika , itakuwa poa sana kutwaa kiatu cha dhahabu kwa mara nyingine tena na nitaendelea kujituma kuanzia sasa mpaka mwisho wa msimu."