Wakatoliki wa jiji la Rome, wameishangaza Barcelona, kwa kuwatungua kwa mapana na marefu 3-0 na kuweza kusonga hatua ya nusu fainali kwa jumla ya 4-4 lakini wakipata wakifuzu kwa goli la ugenini
Edin Dzeko , Danielle De Rossi, Kostas Manolas ndio wameibuka mashujaa wa AS Roma usiku wa leo .
Lionel Messi amebaki akishangaa tu kwa kile kilichotokea uwanjani pamoja na ndugu zake wa Catalan , ama kweli mpira hauna adabu.
Mo Salah na Bobby Firmino wamepeleka kilio kingine cha tatu mfululizo kwa Pep Guardiola na kuwaondoa Manchester City katika mashindano ya UEFA
Liverpool anasonga mbele kwa jumla ya magoli 5-1 baada ya kushinda 3-0 mechi ya kwanza pale Anfield
Pep Guardiola akitoleaa kwenye eneo lake la ufundi na kupelekwa jukwaani baada ya kumtolea maneno machafu mwamuzi wa mechi.