Jina la Kocha Mkuu wa Taifa Stars Salum Mayanga latajwa kati ya Majina ya Makocha wanne wanaotajwa kuifundisha Klabu ya AFC Leopards ya Kenya.
Leopards ambayo kwasasa inanolewa na Denis Kitambi pia Mtanzania ataachana na Klabu hiyo Mwezi Mei na kuungana na kocha Stewart Hall Ambaye Walikuwa wote Klabu Hapo na Wataenda Nchini Bangladesh kuifundisha Klabu ya Saif FC ya Ligi Kuu Nchini humo.
Makocha wanaowania kuinoa AFC Leopards ni Salum Mayanga (Tanzania),Ronalfo Zapata (Argentina),Didier Gomes da Rosa (Ufaransa).
Gomes da Rosa hivi Sasa anaifunza Klabu ya Coffee FC ya Nchini Ethiopia Kabla ya hapo kaifunza Rayon Sports ya Rwanda pia Coton Sports ya Cameroon.
Zapata Amewahi fundisha nchi za Nigeria, Afrika Kusini pia Gabon.
Dennis Kitambi Ataungana na Kocha wake Aliyekuwa Anamsaidia ndani ya Klabu ya AFC Leopards Stewart Hall katika Klabu ya Saif FC huku Bangladesh.