Breaking News
Loading...
Monday, 9 April 2018

Info Post

Goli pekee alilofunga Emmanuel Okwi limeipa vinara wa Ligi Kuu ya Soka ya Tanzania Bara Simba SC pointi tatu muhimu kabisa kwenye mbio za kuwania Ubingwa wa VPL .

Kwa matokeo hayo Simba SC sasa wanafikisha Pointi 52 , sita zaidi ya Yanga SC ambao wamebaki na mchezo mmoja mkononi huku zikiwa zimebaki mechi 8 kwa Simba na 9 kwa Yanga.

Okwi anafunga goli lake la 17 katika ligi ya VPL , matano zaidi ya wale wanamfuatia kwenye orodha ya Ufungaji, John Bocco na Obrey Chirwa.

Na Simba wanapata ushindi dhidi ya Mtibwa pale Morogoro baada ya majiribio ya misimu mitatu.