Adam Salamba na Laudit Mavugo magoli yao yametosha kuipa pointi moja kwa kila timu Kwenye mtanange wa Lipuli dhidi ya Simba SC na mechi hiyo kuisha sare ya1-1 Kwa matokeo hayo Simba SC sasa wanafikisha pointi 59, kumi na mbili zaidi ya mabingwa watetezi Yanga SC ( Pointi 47 ) huku Simba wakiwa wamecheza michezo 3 zaidi ya Yanga.
Lipuli ( Pointi 32, nafasi ya 7 ) wanazidi kujiweka mahala salama kabisa katika msimamo na kupunguza wasiwasi wa kurejea ligi daraja la kwanza msimu ujao na hatimaye kujikita katika ligi kuu ya Tanzania Bara.