.
Magoli mawili ya Luis Suarez, Lionel Messi, Andres Iniesta na Philipe Coutinho yametosha kuipa Barcelona ubingwa wa kombe la Mfalme kwa mara ya nne mfululizo baada ya kuitungua Sevilla 5-0.
Ni mechi ya mwisho ya Copa Del Rey kwa ' Legend ' Andres Iniesta ambaye anatarajiwa kuondoka Barcelona mwishoni mwa msimu huu.
Kocha Ernesto Valverde anatawa taji lake la kwanza akiwa kocha wa Barcelona katika msimu wake wa kwanza .
.
.
Barcelona sasa wanakuwa wametwaa mataji 30 ya kombe la Mfalme baada ya ushindi wa Jana usiku.