Breaking News
Loading...
Tuesday, 10 April 2018

Info Post

Ligi kuu Soka Tanzania bara Vodacom Premier league inaendela tena Leo kwa michezo mitano kupigwa kwenye viwanja tofauti. Wakati Dar es salaam kutashuhudiwa mchezo Mkubwa kati ya Yanga Sc wakiwaalika Singida United kwenye Uwanja wa Taifa mchezo utakaopigwa saa kumi kamili jioni na utakuwa wenye ushindani sana kutokana na matokeo ya awali kwenye mchezo wa Asfc uliowakutanisha na Yanga kutolewa na Singida kwa mikwaju ya Penalty.
Michezo mingine Stand united dhidi ya Majimaji Fc , Mbao Fc dhidi ya Njombe Mji Fc, Tz Prisons dhidi ya Kagera Sugar wakati Mwadui Fc dhidi ya Lipuli Fc.