Faridi Miraji
kocha wa Arsenal Arsene Wenger ambaye ataondoka Gunners mwishoni mwa msimu huu baada ya miaka 22 amepewa ofa ya kuwa Meneja Mkuu katika timu ya Paris Saint-Germain msimu ujao kwa mujibu wa taarifa kutoka Le10Sport.
Kocha Unai Emery alitangaza jana kuwa ataondoka katika kikosi hiko mwishoni mwa msimu huu na Wenger atakuwa sehemu ya mfumo mpya wa PSG ambao unajumuisha Thomas Tuchel kuwa mbadala wa Emery.