Breaking News
Loading...
Monday, 14 May 2018

Info Post

Naby Keita ataigharimu Liverpool kiasi cha Pauni Milioni 52.75 baada ya  RB Leipzig kumaliza nafasi ya sita katika msimamo wa Bundesliga .

Liverpool walikubali kumsajili keita na kumuhamishia Anfield mwishoni mwa msimu huu , makubaliano yaliyofanyika majira ya kiangazi yaliyopita mwaka 2017 lakini ada yake ilikuwa inategemea na nafasi watakayomaliza Leipzig katika msimamo wa Ligi.

Kama klabu hiyo ya Ujerumani ingeweza kumaliza katika nafasi nne za juu za kufuzu kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao basi ada ya keita ingekuwa Pauni Milioni 59.

Kama Leipzig wangemaliza nafasi ya saba au chini ya hapo zaidi basi ada ya Keita ingepungua zaidi mpaka Pauni Milioni 48.

Ushindi wa Leipzig wa 6-2 dhidi ya Hertha Berlin siku ya Jumamosi ulitosha kwa klabu hiyo kumaliza nafasi ya sita na kupata nafasi ya kucheza mashindano ya Europa Msimu ujao.

Keita amecheza mechi 39 katika mashindano yote ndani ya Leipzig msimu huu ,akifunga magoli 9 na kutengeza magoli 7.