Wiki hii Ligi kuu ya Uingereza itathibitisha kwamba dirisha la usajili la majira ya kiangazi litafunguliwa mapema kabisa siku ya Alhamisi Tarehe 17.05.2018 ili kuendana na sheria za FIFA.
Kanuni za shirikisho la soka Duniani ( FIFA ) zinasema kwamba kila ligi inatakiwa angalau iwe na dirisha moja la usajili katika mwaka wa Kalenda kwa wiki 12.
Mapema msimu huu walikubaliana kwamba dirisha la usajili litafungwa Agosti 9 badala ya kawaida ya Agosti 31, ili kusaidia klabu kukabiliana na usumbufu ndani ya vikosi vyao pindi msimu wa ligi utakapoanza Agosti 11.
Ili kuhakikisha muda unakuwa wa kutosha kwa ligi zote , FIFA sasa wamewataka Ligi kuu ya Uingereza kuharakisha tarehe ya ufunguaji wa dirisha la usajili haraka iwezekanavyo.
Wanatarajiwa kutangaza hayo mabadiliko rasmi Jumatano jioni ambapo vilabu vitaruhusiwa kununua na kuuza wachezaji kuanzia Alhamisi.