Breaking News
Loading...
Wednesday, 9 May 2018

Info Post

Hakika hali ndani ya Kikosi cha Yanga inaonekana wazi si nzuri hasa kwa wachezaji kwani kila siku yamekuwa yanaibuka mambo mapya.

Beki wa kushoto wa Timu ya Yanga ameibuka na Kauli ambayo imewaacha washabiki wengi midomo wazi mara baada ya kuandika Ujumbe ambao unaashiria akishalipwa na Yanga basi anaachana nao.

Haji Mwinyi ni moja ya wachezaji ambao inasemekana mkataba wake unaisha msimu huu, na aliwahi kuhusishwa kuhitajika na timu ya AFC Leopards ya KENYA.

Kupitia Ukurasa wake wa Instagram Haji aliandika

” Zanzibar ndio home nilipe nisepe sheria msumeno mwanzo mwishooo mngwali “

Baada ya Kauli hiyo washabiki wanaoaminika kuwa ni wa Yanga walimcharukia