Arsene Wenger ameelezea nia yake ya kuendelea kufundisha soka na amesema kwamba amepokea ofa nyingi tofauti na alivyotegemea.
Wenger ameng'atuka wadhifa wake wa kuwa kocha wa Arsenal baada ya miaka 22 mwishoni mwa msimu huu , na kwa kipindi chote hiko amefanikiwa kutwaa mataji matatu ya Ligi kuu ya Soka ya Uingereza na rekodi ya kutwaa mataji saba ya kombe la FA.
Akiongea kuelekea mechi ya EPL dhidi ya Leicester City siku ya Jumatano Wenger ameulizwa kama ametafutwa kuhusu ofa za kazi mahala pengine.
. " Ndio, zaidi na nilivyotegemea."
. " Lakini sifanyii tathimini wala kuzifikiria kwa sasa. Nataka kufanya kazi vizuri hapa mpaka siku ya mwisho ya mkataba wangu . Bila shaka nitafanya kazi tena. Ubongo wangu unahitaji kazi ."
. " Nina uzoefu mkubwa sana kwenye utawala kiujumla . Kwahiyo nitafanya kazi . Kazi gani nitafanya sijui bado."
Alipoulizwa zaidi kama atafanya kazi katika klabu nyingine ya Uingereza , Wenger amesema," Kwasasa , hiyo ni ngumu kwangu . kwasasa sioni uwezekano huo ."