Roberto Mancini amekubali kuwa mwalimu mpya wa timu ya taifa Italia akirithi nafasi ya Gian Piero Ventura.
Mancini amekubali kuwa kocha kwa miaka miwili na mkataba utasainiwa rasmi kesho.
Italia imefeli kufuzu kombe la dunia mwaka huu na Ventura akajitoa kwenye nafasi hiyo na tangu hapo wamekuwa wakiangalia ni nani atakayeweza kuchukua mikoba hiyo.
Majina kama Carlo Ancelotti na Antonio Conte yalikuwa yakitajwa kama wenye nafasi kubwa ya kutawazwa kama kocha mpya.
.
Mancini ndiye aliyeongoza Man City kubeba ubingwa wa EPL 2012, pia aliipa Ngao ya hisani na kombe la FA moja kwa miaka minne aliyokaa Etihad kuanzia 2009-2013
Juni 2017 alijiunga na Zenit Saint Petersburg ambapo jana walivunja mkataba kwa makubaliano ya pande zote mbili.