Breaking News
Loading...
Tuesday, 15 May 2018

Info Post

Arsenal kumnasa Seri ?

Mabosi wa klabu ya Arsenal wamefanya mazungumzo na wawakilishi wa kiungo Jean Michael Seri  wakiwa kwenye harakati ya kunasa saini yake majira ya kiangazi, kwa mujibu wa taarifa kutoka Sky Sports.

Wapinzani wao wa London Chelsea nao wanamuwinda kiungo huyo ambaye ana thamani ya Pauni Milioni 40 na alikaribia kusaini ndani ya Barcelona majira ya kiangazi yaliyopita .

Mkurugenzi wa Michezo wa Arsenal, Raul Sanllehi ambaye aliitumikia Barcelona kwa miaka 14 amefungua tena mazungumzo na wakala yule yule aliyefanya nae mazungumzo mwaka jana ambaye ana muwakilisha mchezaji huyo .

Sanllehi anamkubali sana Seri lakini dili lolote litachelewa mpaka pale Arsenal watakapoajiri kocha mpya.
Seri kwa sas anakipiga klabu ya Nice ya Ufaransa na timu ya taifa ya Ivory Coast.