Breaking News
Loading...
Friday, 18 May 2018

Info Post

Na: DANIEL S.FUTE

Inaendelea.... HADI kufikia sasa zimesalia siku 26 kuanza kwa fainali za Kombe la Dunia, huko nchini Urusi.

Inasemekana kwamba hadi kufukia sasa hali ya nchi ya Urusi tayari imeongezeka,  kutokana na watu mbalimbali kuja kuweka makazi yao kwa muda wa mwezi mmoja kwaajili ya fainali hizo.

Hii ni faida kubwa sana kwa taifa la Urusi, maana msimu huu nchi hiyo itakuwa kivutio na itaongeza pato la taifa kupitia fainali hizi. 

Leo tunasonga tena na kiwanja cha nane, baada ya Rostov Arena tulicho kizungumzia siku ya jana.

Samara Arena

Samara Arena ni jina la uwanja ambao upo katika mji wa Samara nchini Urusi. Uwanja huu ulijengwa na Serikali ya mji wa Samara, maalumu kwa fainali za Kombe la Dunia.

Lakini Uwanja wa Samara una jina lake maalumu tofauti na hili la Samara. Uwanja huu unaitwa 'Cosmas Arena'. Kwanini watu wanauita Samara baada ya Cosmas ni kulingana na mji ambao uwanja umejengwa.

Mipango ya kuanza kujenga Uwanja huu ni baada ya mji wa Samara kuchaguliwa kwamba, ni moja ya mji ambao zitafanyika mechi za Kombe la Dunia. Uwanja ulianza kujengwa mwaka 2014 na ukapangwa kumalizika mwaka 2017.

Moja ya kivutio cha Uwanja huu ni eneo la juu la Uwanja wa Samara, kuna paa lenye dome la 65.5 kwenda juu ambalo linaunda paneli 32.

Baada ya kukamilika kwa Uwanja huu, klabu ya Fc Krylia Sovetov Samara ulikabidhiwa kujiendesha kwa matumizi ya mechi za nyumbani kwa klabu hiyo ya Ligi kuu.

Uwanja wa Samara una uwezo wa kuingiza idadi ya watu 44,918. Uwanja huu unatarajiwa kuchezewa mechi sita tu katika fainali hizi zitakazoanza mwezi ujao:

★17 June 2018 16:00 – Costa Rica vs Serbia – Group E

★21 June 2018 19:00 – Denmark vs Australia – Group C

★25 June 2018 18:00 – Uruguay vs Russia – Group A

★28 June 2018 18:00 – Senegal vs Colombia – Group H

★2 July 2018 18:00 – 1E vs 2F – Round of 16

★7 July 2018 18:00 – W55 vs W56 – Quarter Final

Hizi ndizo mechi ambazo zitachezwa hapo katika Uwanja wa Samara Arena, Usikose tena siku ya Jumatatu kwa muendelezo wa makala hii.