Mbwana Samatta jana ameifungia klabu yake ya KRC Genk bao muhimu baada ya kuingia dakika ya 54 akichukua nafasi ya mshambuliaji Nikolaos Karelis huku timu yake ikiwa nyuma kwa bao 1-0 ambapo alisawazisha goli hilo dakika ya 66 hivyo kuinusuru klabu yake na kichapo kutoka KAA Gent.
Mchezo huo ulikua ni wa play off kwa ajili ya kuwania nafasi ya kucheza michuano ya UEFA Europa League na UEFA Champions League msimu ujao.