Barcelona rasmi wamemuarifu beki Aleix Vidal kwamba hatokuwa sehemu ya kikosi chao msimu ujao , kwa mujibu wa taarifa kutoka Mundo Deportivo.
Vidal ambaye alijiunga na Barcelona kutoka Sevilla mwaka 2015, katika misimu miwili iliyopita alikuwa akihusishwa na kuondoka Nou Camp .
Mundo Deportivo limearifu kwamba Vidal angependa kurejea katika klabu yake ya zamani, Sevilla ambao walikuwa wanakaribia kumsajili tena mwezi Januari mwaka huu.
Hata hivyo hawakutaka kufikia ada ambayo Barca walikuwa wanataka ya Euro Milioni 12 na wenyewe walitoa ofa ya kati ya Euro Milioni 7 mpaka 8.