Arsenal wanataka kumuajiri Massimiliano Allegri au Luis Enrique kuwa kocha wao mpya lakini makocha hao wote wawili wana wasiwasi kuhusu mfumo wa Utawala ndani ya Arsenal.
Arsenal wamemuajiri Mkuu wa Mahusiano wa Soka , Raul Sanllehi na Mkuu wa Kitengo cha Usajili Sven Mislintat mwaka Jana na kocha mpya atalazimika kufanya kazi karibu kabisa na watu hao wawili.
Mikel Arteta naye bado anahusishwa kwa karibu sana kurithi mikoba ya Wenger . Nahodha huyo wa zamani wa Arsenal kwa sasa ni kocha msaidizi wa Manchester City.