Breaking News
Loading...
Monday, 7 May 2018

Info Post

Lyon wamekubali kumuuza Nabil Fekie kwenda Liverpool pindi dirisha la usajili litakapofunguliwa katika dili ambalo linaripotiwa kugharimu kiasi cha Pauni Milioni 61.7, kwa mujibu wa taarifa kutoka RMC Sport.

Kocha wa zamani wa Liverpool , Gerard Houllier, ambaye kwa sasa amekuwa mshauri wa Mwenyekiti wa Lyon, Jean-Michel Aulas,ameripotiwa kuwa daraja la dili hilo.

Hata hivyo baada ya ushindi wa 3-0 wa Lyon dhidi ya Troyes, Aulas aliiambia Le10Sport: " Hakuna mawasiliano na Liverpool leo . Nimeshangazwa na hizi taarifa . Hakuna makubaliano yoyote katika mkataba wa Nabil ambayo yanaelekeza kuondoka kwake."

. " Kiufupi, pindi aliposaini mkataba wake, nilimuambia wakala wake - ambaye nina mahusiano naye mazuri sana kwamba siku ambayo Nabil atataka kuondoka kama nilivyofanya kwa Alexandre Lacazette, Corentin Tolisso au  Karim (Benzema) inabidi aje kuniona mimi "