Mabingwa Wa Soka nchini Tanzania Yanga Sc na wawakilishi pekee wa mashindano ya kimataifa wametoshana nguvu na Timu ya Rayon Sports kutokea Rwanda kwa kutoshana sare ya kutokufungan ndani ya dakika tisini .
Mchezo huo ulioanza kwa kasi kubwa kwa pande zote mbili na kosa kosa kwa timu zote huku Rayon Sports ikikosa kumalizia nafasi nyingi za wazi walizozitengeneza kwenye mchezo huu.
Mpaka sasa Yanga imefikisha Point 1 pekee kwenye michezo miwili waliocheza mpaka sasa huku kundi lao likiongozwa na Usm Alger ukiwa na point 4 ikifuatiwa na Rayon Sports na Gor Mahia zikiwa na point mbili kila moja