Breaking News
Loading...
Thursday, 3 May 2018

Info Post



Kelvin Patrick Yondani, maarufu kwa jina la utani ‘Cotton Juice’ amesimamishwa kwa muda usiojulikana kucheza Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa kosa kumtemea mate beki Mghana wa Simba SC, Asante Kwasi katika mechi ya mahasimu jadi Aprili 29, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Hayo yamefikiwa katika kikao cha Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi, maarufu kama Kamati ya Saa 72 kilichofanyika juzi mjini Dar es Salaam chini ya Mwenyekiti wake, Clement Sanga ambaye pia ni Kaimu Mwenyekiti wa Yanga kupitia matukio mbalimbali ya Ligi Kuu.

Katika mchezo ambao bao pekee la beki Erasto Edward Nyoni liliipa Simba SC ushindi wa 1-0, Yondan anadaiwa kumtemea mate Kwasi kwa na kusimamishwa kumezingatia Kanuni ya 9(5) ya Ligi Kuu kuhusu Usimamizi wa Ligi.