Breaking News
Loading...
Wednesday, 9 May 2018

Info Post


Nyota wa Crystal Palace,Wilfried Zaha ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Aprili wa Ligi kuu ya soka ya Uingereza.

Zaha mwenye umri wa miaka 25 amefunga magoli manne na kutengeneza moja  ambapo Palace ameshinda mechi mbili na kutoa sare mbili katika mechi nne za mwezi huo.

Zaha ametwaa tuzo hiyo ndani ya Palace na kwa mara ya mwisho mchezaji wa Palace kutwaa tuzo hiyo alikuwa ni Straika Andrew Johnson mwaka 2004.

Zaha amewapiku wachezaji wengine ambao ni Pierre-Emerick Aubameyang, Christian Eriksen, Jake Livermore, Jordan Pickford, Paul Pogba na Raheem Sterling.