DANIEL S.FUTE
TIMU 32, Viwanja 12 na Mechi 62. Hizi ni fainali za Kombe la Dunia mwaka 2018, ambazo zinatarajia kuanza mwezi ujao huko nchini Urusi.
Kabla ya kuanza kwa fainali hizi, nahitaji nikuletee makala fupi kuhusu viwanja 12 ambavyo vitatumika katika fainali hizi huko nchini Urusi na nitakuwa nazungumzia kiwanja kimoja kimoja mpaka vikimalizika vyote 12 pamoja na mechi ambazo zitachezwa katika viwanja hivyo.
Leo nitaanza na kiwanja ambacho kitafungua fainali hizi na ndicho kitafunga fainali hizi, yaani mchezo wa fainali utapigwa hapo.
*Luzhniki Stadium*
Luzhniki ni Uwanja ambao upo katika mji wa Moscow, Wilaya ya Khamovniki. Uwanja huu ulifunguliwa mwaka 1956 kabla ya kuanza kuupanua tena ambapo ulifungwa kwaajili ya matengenezo na ukafunguliwa mwaka 2017, ukiwa na idadi ya kuingiza watu 81,000.
Uwanja huu unatarijwa kuchezewa mechi saba tu katika fainali za Kombe la Dunia, mechi hizo ni:
★14 June 2018 18:00 – Russia vs Saudi Arabia – Group A
★17 June 2018 18:00 – Germany vs Mexico – Group F
★20 June 2018 15:00 – Portugal vs Morocco – Group B
★26 June 2018 17:00 – Denmark vs France – Group C
★1 July 2018 17:00 – 1B vs 2A – Round of 16
★11 July 2018 21:00 – W59 vs W60 – Semi Final
★15 July 2018 18:00 – W61 vs W62 – Final
Hizo ndizo mechi ambazo zitachezwa hapo Luzhniki, Usikose tena hapo kesho na muendelezo wa makala hii.