Arsenal wamehusishwa na usajili wa kiungo Marouane Fellaini na watafanya mazungumzo na kiungo huyo siku ya Jumatano kwa mujibu wa taarifa kutoka The Times.
AC Milan nao wameonesha nia ya kutaka kunasa saini ya kiungo huyo wa kimataifa wa Ubeligiji majira haya ya kiangazi , ambaye mkataba wake na Manchester United unafikia tamati mwezi huu.
Manchester United walikuwa wanataka kumpa mkataba mpya lakini mazungumzo hayo yamesitishwa baada ya kambi ya Fellaini kuhitaji muda wa kuchanganua ofa kutoka klabu zingine na pia kuwa na wasiwasi kuhusu kucheza mara kwa mara katika kikosi cha United msimu ujao.