Winga wa Liverpool Sadio Mane ni windo la usajili la Real Madrid majira haya ya kiangazi na alikuwa kwenye orodha ya usajili ya kocha Zinedine Zidane, kwa mujibu wa taarifa kutoka Marca.
Mane alionesha kiwango kizuri sana kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya akifunga goli la kusawazisha na kugongesha mwamba na imearifiwa kwamba nyota huyo wa kimataifa wa Senegal atakuwa kwenye mawazo ya Real dirisha hili la usajili pindi kocha mpya atakapoajiriwa pale Bernabeu.
Kuondoka kwa Zidane kumeleta kizuizi kiasi katika harakati za kumnasa Mane ambapo Marca na AS yamearifu kwamba tayari Zizou alikuwa ameshaamua kumnasa Mane lakini sasa Uongozi wa Real Madrid bado hauna uhakika kama kocha mpya atataka kuendeleza mpango wa kumnasa winga huyo wa Liverpool.