Kiungo Yaya Toure yupo tayari kucheza kwa mahasimu wa Manchester City, nao ni Manchester United msimu ujao ili kumuonesha Pep Guardiola kwamba amekosea .
Wakala wake Yaya Toure amesema kwamba mteja wake anaweza kubaki ligi kuu ya Uingereza msimu ujao na kucheza katika klabu yoyote ya vilabu sita bora Uingereza ikiwemo Man United.
Toure anahitajika na vilabu nje ya Uingereza pamoja na Major League Soccer klabu ya New York City FC lakini Seluk amesema kwamba mteja wake anataka kumuonesha Guardiola kwamba amekosea na angependa kubaki Uingereza ili kucheza dhidi ya Guardiola hasa baada ya kumshutumu kwamba ana ubaguzi na wachezaji kutoka bara la Afrika.
. " Yaya amepokea ofa nyingi kutoka nchi kadhaa , tena ofa za fedha nyingi , lakini tumeamua kwamba msimu ujao ni kwa ajili ya Guardiola." Seluk ameiambia sport24 . .
. "Kuwahakikishia Mashabiki wa Man City kwamba Toure hajaisha katika Soka , bado ana nguvu na uimara wa kimwili kuweza kucheza katika ligi kuu ya Uingereza."
. " Katika muda ambao vilabu vya Uingereza vinatumia fedha nyingi katika usajili , rasmi nasema hadharani kwamba Yaya yupo tayari kuhamia katika klabu yoyote iliyo ndani ya vilabu sita bora kama mchezaji huru na mshahara wa Pauni Moja tu kwa wiki . Kuwepo tu na mfumo wa bonasi ya mafanikio."
. " Nafikiri mchezaji kama Yaya Toure anaweza kuwa msaada mkubwa kwa vilabu kama Man United, Chelsea, Liverpool, Arsenal au Tottenham . Yaya ni mshindi."
. " Mchezaji yoyote wa daraja la juu mwenye ubora wa Uongozi hawezi kuwa ongezeko baya kwenye kikosi, hasa akiwa haitaji malipo."