Na: DANIEL S.FUTE
MWAMUZI Aden Marwa, kutoka Kenya ambaye aliteuliwa na FIFA kuwa mwamuzi wa kwanza kutoka Afrika Mashariki kucheza fainali za Kombe la Dunia 2018, ameondolewa katika nafasi hiyo.
FIFA imeamua kumuondoa mwamuzi huyu baada ya kupokea rushwa, ili aamue matokeo ya mchezo wa Ligi Kuu ya Kenya. Rushwa hiyo ilikuwa ya mtego kutoka kwa mwandishi wa habari za kiuchunguzi wa Ghana, Anas Aremeyaw.
Marwa alipokea rushwa ya kiasi cha dola 600 za kimarekani. Hivyo mwamuzi huyu hatakuwa katika orodha ya waamuzi ambao wataenda nchini Urusi katika fainali za Kombe la Dunia, ambazo zinatarajia kuanza Juni 14.