Breaking News
Loading...
Thursday, 7 June 2018

Info Post

Nusu Fainali ya Michuano ya SpotPesa Super Kupigwa hii Leo Kwa Michezo yote Miwili katika Uwanja wa Afraha,Nakuru huko Kenya.

Ambapo Katika hatua hii Wawakilishi Wawili kutoka Tanzania Wamefika katika hatua hii Vile Vile Wawakilishi Wawili Kutoka Kenya Wamefika katika hatua hii.


Mapema Saa Saba (7) za Mchana Wawakilishi wa Tanzania Katika Michuano hiyo Simba SC Wanashuka Dimbani Kukipiga Dhidi ya Kakamega Home Boys.

Simba Wamefika hatua hii Kwa Kwatupa Nje Kariobangi Sharks Kwa Mikwaju ya Penati huku Kakamega Home Boys ya Kenya Wamefika katika hatua hii Kwa Kwatupa Nje Yanga SC ya Tanzania Ndani ya Dakika 90.

Mshindi wa Mchezo huo Moja Kwa Moja Anatinga Fainali hiyo na Kumsubiri Mpinzani Wake katika Mchezo Unaofuata.

Nusu Fainali ya Pili Pia Wawakilishi wa Tanzania Singida United Watakuwa Kibaruani kuwavaa Miamba wa Kenya Klabu ya GOR Mahia, Mchezo huo Pia Utapigwa Katika Uwanja wa Afraha,Nakuru huko huko Kenya Alasiri ya Saa 9

Singida United Wamefika katika hatua hii Kwa Kuwafurusha AFC Leopards ya Kenya Kwa Mikwaju ya Penati huku GOR Mahia nao Wamefika katika hatua hii Kwa Kuwatupa  nje JKU FC ya Zenji Ndani ya Dakika 90.

Mshindi wa Nusu Fainali hii ya Pili nae Atatinga Kucheza Fainali na Mshindi wa Nusu Fainali ya Kwanza.

Hapo Utaona tofauti ya  timu za Kenya na Kwetu Tanzania kuwa wao wanaamua Mechi Dakika 90 sisi tunabana Mpaka Mikwaju ya Penati.

Hasiyejipanga leo Mapema tu Anarejea Nyumbani...

#SportPesaSuperCup