Breaking News
Loading...
Monday, 4 June 2018

Info Post

Shirikisho la soka barani Ulaya UEFA limemfungia mechi moja kocha wa Manchester City Pep Guardiola baada ya kutolewa nje na mwamuzi wa pambano la robo fainali ligi ya mabingwa Ulaya dhidi ya Liverpool pale Etihad.

Guardiola alitolewa baada ya kupingana na maamuzi wa mwamuzi Antonio Mateu Lahoz  baada ya kukataa goli la Leroy Sane kipindi cha kwanza katika mechi hiyo.

Liverpool wenyewe wamepigwa faini ya Pauni 17,500 kutokana na fujo zilizotokea katika mechi ya kwanza ya robo fainali ya UEFA dhidi ya City , pamoja na kushambulia gari la Manchester City mwezi Aprili jijini Liverpool.