Kila goli litakalofungwa na Neymar au Lionel Messi katika mashindano rasmi ya kimataifa , ikiwemo fainali za kombe la Dunia nchini Urusi itakuwa ni sawa na Milo 10,000 katika shule kwa ajili wa watoto kule Latin America na Caribbean.
.
.
Kampuni ambayo inasimamia mpango huo ni MasterCard na ilitangaza jana Alhamisi kwamba watachangia Milo 10,000 ya Shule kwa United Nations World Food Program (WFP) kila mara pale Neymar au Messi wakifunga goli.
.
. " Najivunia sana kuwa sehemu ya Kampeni hii , nitasaidia kubadilisha maisha ya maelfu ya Watoto na ni matumaini yangu kwamba italetea tabasamu la kutosha ."
.
.
Neymar yeye kasema," Tunataka kuhakikisha kwamba watato wanapata sahani ya chakula na matumaini zaidi. Pamoja tunaweza kupigana na kuishinda njaa."