Mkuu wa kitengo cha usajili wa Arsenal Sven Mislintat na kocha wa Paris Saint-Germain Thomas Tuchel bado wanafanya mawasiliano na winga wa Barcelona Ousmane Dembele, kwa mujibu wa taarifa kutoka l'Equipe .
.
Jina la winga huyo limekuwa kwenye vyombo vya habari hivi katika siku chache zilizopita , ambapo Liverpool nayo imekuwa klabu ya mwisho kuhusishwa na Mfaransa huyo .
.
.
Licha ya kwamba Mfaransa huyo bado anawasiliana na Mislintat na Tuchel hana mpango wa kuondoka Barcelona licha ya kuwa na msimu wake wa kwanza ambao haukuwa wa kuridhisha .