Breaking News
Loading...
Friday, 15 June 2018

Info Post

Mashabiki wa Nigeria wamepigwa marufuku kuingia uwanjani na  kuku wa 'Bahati ' katika mechi za fainali za kombe la Dunia nchini Urusi kuanzia mechi yao ya ufunguzi dhidi ya Croatia 
Mashabiki wa Super Eagles wanaamini utamaduni wa kuingia na Kuku uwanjani unaleta bahati katika timu.
Hata hivyo Serikali ya Urusi imepiga marufuku utamaduni huo pindi Nigeria watakapocheza mechi yao ya kwanza ya kundi D siku ya Jumamosi.

. " Mashabiki wa Nigeria wameuliza kama inawezekana kuingia na Kuku wazima uwanjani . Tumewaambia kwamba haiwezekani " Waziri wa Utamaduni,  Andrei Ermak amesema hivyo.

Ermak  ameongeza kwamba Wizara yake itawaambia mashabiki wa Nigeria ni Maeneo gani wataruhusiwa kwenda na Kuku wakiwa wanashabikia timu yao.