Ni mwezi ambao tayari tupo ndani ya mfungo wa mwezi mtukufu
wa Ramadhani na Dunia yote macho na masikio yameelekezwa katika bara la Amerika
ya Kusini katika nchi ya Brazil ambako kuna fainal za kombe la dunia la mpira wa miguu maana ya soka,ni
balaa watu wanakesha usiku kucha wakipigwa na mmbu kisaa tu ni soka.
Soka au mpira wa miguu ni mchezo wa
ajabu mno,ni mchezo ambao unaweza kuleta furaha wakati wote na unaweza ukaleta
maafa wakati wowote,kwangu mimi naona ni mchezo katili na wenye roho mbaya muda
wote,kwa watu ambao ni vichaa kabisa wa soka ni nadra mno machozi
kutokupatikana uwanjani,ndugu yangu Maico Richard Wambura ataungana na mimi
kuwa soka ni mchezo katili.
Bahati mbaya nimezaliwa na kujikuta
natumbukia katika ukichaa wa soka,watu wengi wananijua na kunifahamu kupitia
iwe wakati nacheza,nikiwa kocha,nikiwa mchambuzi au nikiwa naandika
makala,nimejikuta niko chizi tu wa soka.
Mchezo wa soka ni kama Dini tofauti na
dini ni kwamba soka kila mtu analiangalia na kulisema anavyojua,Rais wa Fifa
Sett Blarte anasema utamu ni kuzungumzwa mchezo unachezwa dakika 90 lakini
unazungumzwa wakati wote,matukio yeyote ya ajabu kama Luis Suarez kumg'ata mtu
jino Cristiano Ronaldo kuaga mashindano
kwa goli moja ,bao la Robin Van Persie lilivyokuwa tamu watu hawaelewi
lilitokana na krosi au majaro soka lazima lizungumzwe ndo utamu wake hapo.
Rais wa TFF aliyemaliza muda wake
Leodgar Shilla mwaka jana wakati akiongea katika tunzo la Mwanaspoti la kuchagua wachezaji bora
alizungumzia soka,kitu anachokikumbuka mpaka leo ni jasho lake na harufu ya
viatu yeye na wenzake ndani ya chumba cha kubadilishia nguo wakati wa
mapumziko,ilikuwa ni shashu ya ushindi ndo utamu wa soka huo
Ronaldo de Lima mmoja kati wafungaji
bora waliopata kutokea katika Dunia hii,akikumbuka soka anasema kitu pekee
alichokikosa katika soka kwa sasa ni kushangiliwa na watu wengi kwa mara moja
leo pamoja na utajiri wake lakini hicho amekikosa kimo ndani soka.
Soka ni mchezo na juzi baada ya mchezo
kati ya Ivory Coast kocha wao kijana mdogo kabisa Mfaransa Sabri Lamouchi
alisema kwa masikitiko baada ya mechi kwisha kuwa ulikuwa ni mchezo wa kikatili
mno na kwamba ni kweli Ugiriki walistahili kushinda lakini tungepata faida kama
mechi ingemalizika katika muda wake.Ni maneno ya huzuni kwa upande ulioshindwa
yakisemwa kwa huzuni kubwa mno lakini ni furaha kwa upande mwingine ndio maana
tunasema soka ni mchezo katili.
Katika hali ya kawaida kabisa Nchi nzima
ya Ivory Coast na waafrika kwa ujumla walikuwa wamebaki na dakika moja tu
kukamilisha furaha yao mtu mmoja tu Georgios Samaras anaukwamisha mpira kimiani
kwa njia ya penalt inayotolewa na Mwamuzi katika muda mbaya na katika mazingira
hatarishi na hasa kwa viwanja vyetu vya
uswahili,na katika tukio jepesi mnooo,soka ni mchezo katili na mwamuzi anafanya
ukatili wa hali ya juu mno kwa bara zima la Afrika.
Ivory Coast mashindano na wakongwe wake
walioshiriki fainal hizi kwa mara ya tatu ndoto zao za angalau kufika robo
fainal zikiyeyuka dakika moja ya mwisho kweli soka katili,nani alitegemea
kizazi hiki kinachoondoka cha kina Didier Drogba,Yaya Toure,Solomon
Kalou,Gervinho,Kolo Toure kiishie hapo kilipoishia hakuna soka ndio limeamua
hatuna ujanja.
Mexico walijikuta kwenye hali mbaya juzi
mbele ya Uholanzi kama ilivyowakuta Ivory Coast hadi tatu kabla ya mpira kwisha
kwa muda wa kawaida na si wanyongeza walijikuta furaha yao ikiota mbawa kwa
kujapwa magoli mawili ya haraka haraka ikiwepo na penalt ya utata kweli soka ni
mchezo katili.
Wanaoongoza soka ni lazima wajue kuwa
soka ni mchezo hatari,soka ni mchezo unaopendwa mno na kuna watu wamezaliwa
katika soka,wamekulia katika soka,wapo ndani ya soka na maisha yao yote
yanategemea sokaaa,ni lazima wautendee haki mchezo wenyewe,ni lazima wawe
waadilifu,wakweli na wanyenyekevu kwa wanaopenda soka yaani kuanzia
mashabiki,makocha,waamuzi,madactari wa michezo,waandishi wa habari za michezo
na wahusika wote.
Wanaongoza soka wakiutendea haki mchezo
wenyewe,wakatoa haki kila kuanzia kwa makocha kuwaelimisha kwa haki bila
ubaguzi,kutoa gredi za kwa waamuzi anayestahili,waamuzi kuwa Fair ndani ya
uwanja na mashabiki kuwa mashabiki si uhasma huenda soka likabadilika sio
katili mno kama ilivyo sasa,ambapo soka limekuwa katili mno mtu mmoja
anahatarisha maisha ya wengi mno mfano kwa kutoa penalt dakika za mwisho na
ikiwa haina kichwa wala miguu,soka ni mchezo hatari na mchezo katili mnooo