Breaking News
Loading...
Sunday, 7 September 2014

Info Post

Habari zilizoifikia MWAISABULA BLOG zimesema kuwa mtanange uliokuwa upigwe leo kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam baina ya klabu ya Yanga dhidi ya Bullets FC ya Malawi umehairishwa kutokana na timu hiyo ya Malawi kutofika nchini hadi mchana huu.

Kutoka ndani ya chanzo makini ndani ya klabu hiyo ni kuwa bado wapo katika mchakato wa kuwasiliana na viongozi wa klabu hiyo kujua nini kilikwamisha safari yao na hapo ndipo watakapoweza kutoa taarifa rasmi kama watatangaza tena siku nyingine itayopigwa mechi hiyo.