Dennis Odhiambo (kulia) akichuana na Simon Msuva
Nahodha wa klabu ya
Thika United ya Kenya, Deniss Odhiambo ameiambia MWAISABULA BLOG kuwa amevutiwa
sana na klabu ya Yanga na yupo tayari kuitumikia muda wowote watakaihitaji
huduma yake.
Deniss ambaye ni ndugu na Moses Odhiambo aliyewahi kuichezea
Yanga miaka ya nyuma amevutiwa sana na
namna Yanga ilivyocheza kwenye mechi iliyopigwa Jumatano ( September 3 ) kwenye
dimba la uwanja wa taifa ambapo timu yake ya Thika ililala bao 1-0.
“ Nimevutiwa sana na soka ya Yanga, ki ukweli wanacheza
vizuri sana, nipo tayari kuipokea ofa yeyote kutoka kwao” alisema Kiungo huyo
aliyengara katika mchezo huo wa Jumatano.