Breaking News
Loading...
Sunday, 7 September 2014

Info Post

                  MAO MKAMI AKIFANYA MAMBO

LILE BONANZA kubwa linalofanyika kila mwisho wa mwezi  linalohusisha wanasoka wa zamani waliowahi kutamba katika medani ya soka nchini limefanyika leo katika viwanja vya shule ya msingi Buguruni ambapo kwa mwezi huu lilikuwa la lengo la kumuenzi marehemu Gebo Peter.

Akizuingumza na MWAISABULA BLOGU mratibu wa Bonanza ambaye pia ni kiongozi wa Uhuru Veteran Dr Richard Msungu amesema kuwa Bonanza la mwezi huu limejumuisha timu 8 tofauti na awali ambavyo lilikuwa likishirikisha timu 5.

Pia Msungu alitoa wito kwa maveterani wengine kujitokeza kwa wingi katika kushiriki katika Mabonanza kwani ni nafasi nzuri yao wao kujenga afya zao.

Bonanza hilo limedhaminiwa na hoteli ya LEKAM ROYAL LODGE & PUB iliyopo maeneo ya Buguruni.
DR RICHARD MSUNGU, MRATIBU WA BONANZA HILO

BAADHI YA WAKONGWE MBALIMBALI WALIOHUDHURIA BONANZA HILO