
You'll Never Walk Alone, moja ya nyimbo maarufu kabisa katika viwanja vya soka. Nyimbo ambayo pengine inaimbwa na vilabu zaidi ya vitatu duniani lakini hapana shaka ikisikika tu watu hutambua Liverpool wapo uwanjani. Ni nyimbo ambayo maneno yake hukupa imani ya kuvuka mto kwa miguu. Hii uwaleta walevi na wale wasio mahala pamoja, wakorofi na wastaarabu sehemu moja na washika dini kwa wapagani sehemu moja. Ikiimbwa hii kila mmoja uelewa jambo moja tu, Liverpool. Ni nyimbo hii ambayo Simao Sabrosa alibaki akishangaa na asiamini kama timu aloifunga ilikuwa inashangiliwa kuliko yake iliyoshinda, ni sababu hii ambayo Thiery Henry aliwahi kukiri Anfield ni sehemu
ambayo yeye hupenda kucheza. Naamini hata Gerrard ni nyimbo hii ndio inampa sababu kadhaa za kuendelea kuwa pale. Lakini Kuna tofauti moja kubwa katika hii nyimbo nayo ni wakati. Wakati umepita sasa na nyimbo inaimbwa vile vile lakini katika maadhi tofauti. Namna mbili tofauti, wakati kipindi Mike Tyson akiwa ananyanyasa ulingoni na Liverpool ilikuwa moja ya timu ambazo usingejiuliza Mara mbili katika timu mbili bora zaidi Uingereza, wakiwa na ugonjwa wao usiokoma(ukame wa ligi kuu Uingereza) bado walibaki timu iliyotoa mwanga katika upande wa pili(makombe mengine). Walau nyimbo ya YNWA ilikuwa sahihi Sana kutumika, ilitumika kwa ufasaha. Kila siku ungewaza Kuna anga la Dhahabu mbele Yao, walikuwa na upande wa kujipigia kifua kule Ligi ya mabingwa Ulaya.
Umeiona Liverpool ya sasa? Umeitizama inavyocheza? Unamjua mchezaji wao
bora mpaka sasa? Mechi bora walioicheza mpaka Leo ni mechi ya kirafiki
dhidi ya Borrusia Dortmund. Kama Kuna msimu ambao ile nyimbo Yao
ilitendewa haki basi ni msimu ulioisha, na kama Kuna msimu ambao ile
nyimbo ilitakiwa kuimbwa kwa nguvu zaidi basi ni msimu huu. Kuna wakati
inakupasa kujiuliza, tatizo ni nini. Je ni wachezaji wapya? Je ni Suarez
kuondoka? Ama ni Sturridge? Wengi watasema Suarez lakini Liverpool
walijua fika huyu bwana angeondoka, inaweza kuwa shida Sana lakini bado
napata wasiwasi. Ukiitazama Liverpool ya sasa unapata zaidi ya maswali
10 kwa wakati mmoja. Lakini maswali yote kwa wale wasiopenda shida
anaweza kukujibu kwa namna moja tu, MTIZAME KOCHA. Hata Mimi nimewaza
hivyo pia acha nimtizame Brendan Rodgers. Najaribu kujiuliza je ni
huyuhuyu aloitengeneza Liverpool iliyokuwa inamaliza michezo yake katika
kipindi cha kwanza? Ni huyu alokosa ubingwa kutokana na kuteleza kwa
kipenzi cha washabikibwa Liverpool? Kwa kuwa yupo mbali ikabidi nitizame
mwenendo wake ili nijipe Majibu sahihi mwenyewe.
Kama Kuna meneja ambaye aliingia msimu mpya akiwa na Imani kubwa basi
hapana shaka jina la Brendan Rodgers litakuwa miongoni mwa wale
waliokuwa wanaongoza hiyo orodha. Huitaji akili nyingi kujua hili.
Brendan aliamini ametengeneza filosofia ambayo iliwatesa na ingeendelea
kuwatesa wapinzani. Ni filosofia ambayo wachache ufanikiwa nayo haswa
kama Una mchezaji mwenye jina kubwa klabuni. Brendan Rodgers aliamini
ametengeneza "free flowing team" yaani timu yenye mtirirko huru na ndio
maana si ajabu kuona kuwa alikuwa na washambuliaji waliofunga magoli
mengi zaidi na akawa na beki aliyefunga goli nyingi zaidi. Kwake jukumu
la mchezaji la awali lilikuwa ushambuliaji na sio uzuiaji na ndio maana
Sio ajabu kuona mchezaji aliyekuwa anatumika kama kiungo wa Ulinzi
kuongoza orodha ya waliosaidia upatikanaji wa magoli mengi katika ligi.
Hapa Rodgers aliamini kaweza, hata Mimi niliamini hivyo, hapana shaka
hata wewe msomaji pia. Ungempinga vipi wakati ameshakuonyesha uwanjani?
Kama Kuna vitu Liverpool walishavijua vinakuja basi ni suala la Luis
Suarez kuondoka. Hapa ndipo hesabu za Rodgers katika wepesi zaidi
zilipoanzia. Katika kalamu na karatasi yake alijiuliza kilichowanyima
ubingwa msimu uliopita, Jibu akapata jepesi kabisa na haraka, ilikuwa
safu yake ya ulinzi. Kisha akatizama timu yake ilifunga magoli mangapi
akagundua kuwa kama angeondoa magoli ya Suarez Liverpool bado ilikuwa
inasalia kuwa timu ya pili nyuma ya Man City kwa magoli mengi. Hapa
ndipo maamuzi yake SAHIHI yalipokuja. Mtu wa muhimu kabisa wa kuziba
pengo la Suarez alitakiwa kwanza atoke katika safu ya Ulinzi, Kisha
alihitaji mtu wa ushambuliaji ambaye angeweza kumpatia magoli walau
16/18 maana yake anagalu nusu ya alofunga Suarez. Hapa ndipo mawazo ya
aina ya kina Falcao yakapotea, aliamini aina hii ingetaka itizamwe
yenyewe kabla ya timu jambo ambalo lingeharibu utaratibu. Na katika
ulinzi apunguze magoli ya kufungwa walau kwa nusu yabaki 25 kutoka 50.
Hapa Liverpool ingefunga magoli machache kuliko msimu uliopita lakini
wangekuwa na wastani mzuri wa tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa
kuliko msimu uliopita. Hapa ndipo Rodgers alipofungia mahesabu na
kuamini kuwa ameandaa mtihani mpya ambao wapinzani ungewatoa jasho.
Pamoja na kwamba wasahishaji wangekuwa hao hao ila kuyajua Majibu yake
ingekuwa ngumu Sana. Hapa akafungua pochi akaelekeza nguvu katika maeneo
yenye shida zaidi, ulinzi na kiungo basi akaitafuta fukwe ya Miami
ilipo huki taratibu akisubiri kuamua Kati ya Balloteli na Remy nani
aingie. Bahati mbaya alisahau vitu 3 vya msingi. Tatizo kubwa la ulinzi
lilikuwa kiungo mkabaji wa asili( Heshima kwa Gerrard ndio dhambi
pengine inayomtafuna), Kiwango na matumizi ya Henderson(huyu ndio
alikuwa nguzo ya Liverpool) pia hakukumbuka Afya ya Sturridge. Hapa
ndipo mtihani wake ulipovuja, hapa ndipo kila meneja amepata Majibu,
bahati mbaya hakuna muda wa kutunga mwingine, na hii ndio adhabu ya
kalamu yake mwenyewe.
Unamfahamu Napoleon Bonaparte moja ya viongozi wenye roho ngumu na ya
kigaidi kuwahi kuiongoza Ufaransa. Aliwahi kusema " Dini ndio sababu
inayowafanya masikini wasiue matajiri" hapa ndipo mashabiki wa Liverpool
walipo. Wanaishi katika dini yenye imani kali, wameishi wakiamini Kuwa
Huwezi Kutembea Peke Yako, ukiharibu tumeharibu wote. Nyimbo ya YNWA ni
msingi mkubwa unaowaongoza, bahati mbaya mdomo unaimba lakini rohoni
wengi wanatamani kumuazima Roman Abramovich utendaji. Usahihi wa hii
nyimbo sio wakati huu, sio wakati ambao Liverpool inafungwa mechi tano
mfululizo. Usahihi wake ni kama msimu uliopita unaimba ukiamini
ukifungwa Leo utafurahi katika mechi 7 au 8 zijazo. Hata Bob Peasley na
Bill Shankly makocha waliotengenezewa sanamu katika malango ya uwanja
waliweka utaratibu huu. Brendan Rodgers anaishi katika kivuli hiki, dini
hii ina utaratibu unaomlinda. Utaanzaje kwenda na bango la Brendan Out
wakati kabla na baada ya mechi unaimba You'll Never Walk Alone.( hutokaa
utembee mwenyewe). Lakini kila nikitizama mwenendo wa Liverpool sidhani
kama yupo salama Sana. Wale wamiliki akina Henry ndio watu pekee ambao
hawaishi katika hii dini, wao wanaamini katika michezo mingine kabisa.
Ningekuwa na uwezo ningemtumia Brendan ujumbe mfupi tu, "UNAIJUA DINI YA
HENRY. Najua jambo la kwanza angekumbuka King Kenny Dalglish. Muda
unaenda na usalama wa Brendan upo katika mikono miwili tu. Ya kwake
mwenyewe na ya wapinzani. Hata hivyo mwandishi maarufu Maggie Ghallager
aliwahi kusema hakuna kazi ngumu kama ya kuwa mwalimu mzuri. Hata
Nyerere hakufanikiwa hapa ndio maana wapo wanaompinga hadharani. Hata
Brendan yupo hapa ndio maana naweza kuyatabiri maamuzi ya John Henry,
naamini hata wewe ushayajua. Tatizo la Brendan ni moja tu mpaka sasa
mtihani alotunga ulivujia kwa wasahihishaji wengine. Sioni Liverpool
ikibadilika karibuni kabla ya kocha hajabadilika.
Ahsanteni
By Nicasius Coutinho Suso
Ahsanteni
By Nicasius Coutinho Suso