Breaking News
Loading...
Friday, 14 November 2014

Info Post


            
           Kama unamini kwenye bahati basi kasome maisha ya Vince Lombard.Hakuna mtu aliyetegemea kuwa Lombard atakuwa mtu wa kukumbukwa kwenye ardhi ya Marekani.Lakini Lombardi aliamini ipo siku juhudi zake zitamfikisha  kwenye ndoto zake.Ndivyo ilivyokua,Mpaka sasa Lombardi anahesabiwa kama kocha bora kuwai kutokea kwenye ardhi ya marekani.Lombardi ni kocha mwenye mafanikio zaidi kwenye ligi ya marekani. Japo watu wengi walikua wanamuhesabu kama mtu mwenye bahati,Lakini Lombardi mpaka anafika alipofika alikua anaamini kwenye kujituma.”Football is like life,It requires Preseverance,Self-denial,Hardwork,Sacrifice,Dedication and Respect for Authority”.(“Mpira ni kama maisha,Unahitaji uvumilivu,kujinyima,Kujitma,kujitoa na kuheshimu mamlaka”).Hiyo ni kauli kuu ya bwana Lombardi katika
mchezo pendwa wa mpira wa miguu. Kauli hiyo ilikuwa ikiwalenga haswa wachezaji wavivu.Bila shaka kauli hiyo ina ukweli mtupu ndani yake. Ukiangalia wachezaji wote waliofanikiwa Duniani lazima wawe na vitu alivyovisema Kocha Lombardi.
            Nashukuru Mungu kwa kuniwezesha kuangalia timu zote zinazoshiriki ligi kuu Tanzania bara msimu huu.Wakati naendelea kuangalia ligi hiyo nilikua naendelea kutafuta wachezaji walioelewa maneno ya hekima ya Lombardi.Mara nyingi nikawa mbaguzi kwa kufuatilia zaidi wachezaji wetu(Watanzania) kuliko wachezaji wa kigeni.Wachezaji wetu wengi  wamepitwa kabisa na busara za bwana Lombardi.Wachezaji wengi,waaliyadanganya macho yangu kwa viwango vyao.Msuva ,Mkude na Ame Ally angalau waliupoza moyo wangu.
             Nikaamua kulitupa jicho langu pia kwa hawa wanaojiita ‘Maprofeshino’.Nikafikiri kuwa wao watanionesha tofauti kidogo.Lakini nikagundua kuwa maprofeshino hao nao wengi  ni waongo.Katika mechi  chache hizi nilizoangalia sikuona haja ya kuwa na wachezaji wa kigeni watano katika timu.Eti Jaja na kwizera nao ni wachezaji wa kulipwa?,Hii ni hatari.Wachezaji hao hawana msaada kwenye timu zao kuwazidi wachezaji wetu wa ndani.Siwezi kumchezesha jaja wakati kuna Tegete na Javu kwenye benchi.Siwezi kumpa nafasi ya hata kukaa kwenye benchi la wachezaji wa akiba mtu kama kwizera.Azam nae wanae ‘Profeshino’ Ismail Diarra ambaye anakula pesa za mzee bakhresa bila kugusa uwanjani.
              Labda kama sielewi maana halisi ya kuwa na wachezaji wa kigeni hapa nchini.Lengo kuu la watu hawa ni kuleta changamoto kwenye ligi yetu na kuwapa changamoto wachezaji wetu.Lakini wengi wao hawana tofauti na wachezaji wetu wa ndani.Matatizo ya wachezaji wengi ni yale yale aliyoyasema bwana Lombardi,Kutokujituma,Kutojitoa,Kutokua na bidii,Kutokuwa wavumilivu na wengine kufikia hatua hata ya kukosa heshima kwa watawala wao.Hakuna mengine zaidi ya hayo.
             Waswahili wanasema kwenye msafara wa mamba hawakosi kenge.Licha ya wachezaji wengi wa timu zetu kukosa mambo muhimu yanayowafanya wasifikie ubora wao,Lakini kuna wachezaji ambao wamekua vioo vya wachezaji wavivu ligi Tanzania bara.Mpaka ligi ilipofika nimemuona mchezaji mmoja tu ambaye ni mfano wa kuigwa kwa wachezaji wetu na hata hawa ‘maprofeshino’.Si mwingine ni Emmanuel Okwi.Mguu wa Okwi hausemi uwongo na wala akili yake haidanganyi hasilani.
           Pamoja na Simba kutofanya vizuri mpaka sasa lakini Okwi ameonyesha tofauti kubwa kati yake na wachezaji wengine.Okwi ni mchezaji anayejituma ,anayejitoa,mvumilivu,mwenye bidii,anayejinyima na pia mwenye heshima kwa mamlaka iliyo juu yake.Kuhusu kujituma na kujitoa kwake bila shaka kila mmoja atakuwa shahidi,Anachofanya Okwi huwa nakifananisha zaidi na anachokifanya Sanchez wa Arsenal.Popota mpira ulipo utamkuta okwi karibu yake.Pale simba wanaposhambulia ujue mpira upo kwenye mguu wa Okwi.Pale Simba wanapofunga goli ujue limefungwa au kutengenezwa na okwi.Hakuna goli la simba lilofungwa bila mchango wa okwi,Kati ya magoli 7 simba ambayo wamefunga,Matatu yamefungwa na okwi,matatu yametengenezwa na okwi pia moja limefungwa kwa mpira wa adhabu baada ya okwi kuangushwa karibu na eneo la hatari la timu pinzani.Kila unapotaja simba lazima utaje jina la Okwi,Kila unapozungumzia ligi kuu Tanzania utakua mchoyo kama hutomzungumzia mwanaume huyu.Pia Okwi amekuwa mvumilivu sana,pamoja na chokochoko zinazoendea klabuni,tena nyingine zikimhusu yeye dhidi ya wachezaji wenzake.Lakini aliziba masikio na kufanya yale yaliyomleta Tanzania ndani ya uwanja.  
            Tatizo linakuja kwa wachezaji wetu wengi kuamini sana kwenye bahati kuliko juhudi.Tena wengi wataacha kuiga mazuri na juhudi  ya Emmanuel Okwi badala yake watakaa chini kutafuta mbinu za kummaliza Okwi.Wachezaji wengi wa Afrika wamejawa na mioyo ya husuda kwa  watu haina ya Okwi.Lakini hiyo haitawasaidia kitu.Wachezaji wetu pamoja na hawa maprofeshino upepo hawana budi kuwa na roho ya kujituma kama aliyo nayo Okwi,Inabidi wabadilike na kuona mpira kama  sehemu ya maisha yao,Kujituma na kuongeza bidii kwao Uwanjani ndio kutawaletea manufaa kwenye maisha yao.Wasipofanya hivo wakubali kuendelea kubuluzwa na profeshino wa ukweli Emmanuel Okwi,Kwani mpaka sasa ni yeye pekee ndie amesikiliza na kuzifanyia kazi nasaaa za Vince Lombardi.
                                                                       Na
                                                             Allen Kaijage
                                                             0655106767