Breaking News
Loading...
Thursday, 5 March 2015

Info Post
Jinamizi la majeruhi limeendelea kuiandama klabu ya Arsenal baada ya kubainika kuwa beki wake mpya Gabriel Paulista atakua nje kwa kipindi kinachokaribia mwezi kutokana na majeraha ya misuli.
Mbrazili Paulista ambaye amelisajiliwa na Arsenal kwenye dirisha dogo la usajili akitokea Villareal ya Hispania alipata tatizo hilo kwenye mchezo baina ya timu dhidi ya QPR jana usiku ambapo Arsenal ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.
Kocha Mkuu wa Arsenal Arsene Wenger amethibitisha kuwa Paulista atakuwa nje ya uwanja kwa kipindi hiko na hivyo kuungana na majeruhio wa muda mrefu Mikel Arteta, Abou Diaby, Mathew Debuchy  na Jack Wilshere.
"Ni tatizo la misuli. Sifahamu , lilikuwa ni tatizo baya ambalo asingeweza kurudi uwanjani. Atakuwa nje kwa siku 21 na sio miaka," alisema Wenger.
Kuumia kwa Paulista kunaweza kuwa pigo kwa safu ya ulinzi ya Arsenal ambayo imekuwa ikiyumba kwenye siku za hivi karibuni.