.
Miezi miwili iliyopita nilitembelea
mitaa ya Kigamboni nikakutana mzee moja mshabiki mkubwa sana wa ile iliyokuwa
Sunderland yaani sasa ni Simba anaitwa Nassoro Mkutuka mtunzi wa mashairi
maarufu kwa jina la Hailati,aliniambia bwa mdogo nenda kaandike makala Kaseja
hawezi kurudi Simba aslani,sikuamini akanisisitizia kuwa kamwe hatotokea
mchezaji kucheza Simba zaidi ya miaka kumi,nikabaki nimeduwaaa,nikavuta hisia
na kuamua kuandika makala hii.
Zamoyoni Mogela ' Golden Boy' alianza
kuchezea Simba akitokea timu ya Taifa mwaka 1982 ,Juma Kaseja alianza kuchezea
Simba 2003 baada ya kusajiliwa
2002,wenye Simba wenyewe wanasema kamwe mchezaji wao hawezi kucheza zaidi ya
miaka 10 na ndivyo ilivyokuwa kwa kina Adamu Sabu,Abdalh Kibaden Mohamedy Mwameja aliyesajiliwa mwaka 1992 na
wengineo.
Mogela ambaye alisajiliwa na wenzake
akina Malota Soma na Sospeter Mwaluko alikuwa kipenzi mno cha mashabiki na
wanachama wa Simba Sports club,aliondoka Simba kwa tuhuma nzito toka kwa
viongozi wa wakati ule akina Juma Salum
na kuwafanya mashabiki kuamini na kumfanya Mogan kupoteza marafiki wake wengi
waliokuwa wakimuhusudu kupita kiasi.
Akisimulia kwa kinywa chake Mogan ambaye
wakati alizushiwa balaa kwa kuwa alikuwa
ni kiongozi wa wachezaji yaani Kapten na
muda wote alikuwa ni mtetezi wa wachezaji wenzake jambo ambalo viongozi huwa
hawalitaki na hawalipendi kabisa.
Uongozi wa wakati huo ambao ulikuwa
ukiongozwa na Mzee Juma Salum na wafadhili wao wakuu kabisa akina Azim Dewj na
Ahmedy Bora walimtuhumu Zamoyoni Mogela kuwa mara zote huwa hawafungi Yanga kwa
kuwa tu anahongwa na Abass Gulamali ambaye alikuwa ni mfadhili mkuu wa timu
hiyo,kitendo kilichomuuma sana mkongwe
huyo ambaye kwake Simba ilikuwa ni sehemu ya familia alicheza kwa moyo
woteee.Capten zamoyoni Mogela akaliacha jahazi mwishoni mwa mwaka 1991
akapumzika nyumbani kwa muda wa Mwaka ndipo upande wa upinzani ukiongozwa
na Waziri wa Fedha wakati ule
akishirikia kwa karibu na mfadhili wao Abass Gulamali na Majid Seif wakannyakua
mtaalamu.
Naiangalia njia hiyo ya Mogan naiona
ndio ya Juma Kaseja leo, akiwa ni kiongozi wa wachezaji kama ilivyokuwa kwa
Zamoyoni Mogela naye pia ni mtetezi wa wenzake jahazi kaliachia , ametua Yanga
Afrikani na kuungana na makipa wenzake aliowahi kucheza nao Simba Ally Mustafa
Barthez na Deogratus Munish Dida ,ametumikia timu ya Simba kwa mapenzi makubwa
mnoo na amekuwa na marafiki wengi ndani ya timu leo anawaacha kwa sababu tu ya
viongozi kumwekea maneno yasiyo yake kama alivyowekewa Zamoyoni Mogela miaka
ile, au ndio kile kivuli cha wazee wale wa Sunderland ,kama ni hivyo
inasikitisha mno.
Alichokifanya Marehemu Abbas Gulamali miaka ile ndicho
alichokifanya Manji leo akiwatumia majemedari wake Seif Magari na Abdalah Bin
Kleb sina hakika na yule aliyekuwa Waziri wa Fedha wakati ule kama na hili
kashiriki maana naona kwa sasa ana majukumu makubwa mno ya Kitaifa.
wengi tulikuwa tunajiuliza nini
kinachowasukuma mashabiki kuruhusu nyota wao waliodumu katika timu kipindi
kirefu lakini iwe mwisho miaka tu,ninini kimefichwa na wazee wale akina Mkutuka
ambacho sisi vijana wa leo hatukijui!!!.
Basi kama ndio hivyo nenda Kaseja
usipinge kauli za wazee hata kama timu unaipenda vipi,hata kama bado una uwezo
wa kiasi gani hapana wazee waliotangulia wanasema Simba mwisho miaka kumi tu ime nimebaki nimeduwaa na kuwaachia
wapenzi wasomaji kufanya utafiti wa kina katika suala .