Breaking News
Loading...
Thursday, 5 March 2015

Info Post
Kagera Sugar wamewatupia lawama waamuzi kuwa ndio chanzo cha wao kufungwa katika mchezo uliopita wa Ligi Kuu dhidi ya Stand United kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.
Akizungumza na mwandishi wetu, Kocha Mkuu wa Kagera Sugar Jackson Mayanja, alisema katika mchezo huo waamuzi walionesha kuibeba wazi Stand United jambo lililowapa wakati mgumu wachezaji wake kucheza soka kwani walitolewa mchezoni.
"Waamuzi waliamua kwa makusudi kupindisha kanuni na sheria za soka ili timu waliyoitaka wao ishinde. Stand siyo kama wana kikosi kizuri ila wamekuwa wakitumia mbinu chafu za kuwatumia marefa pindi wanapokuwa nyumbani. Naomba TFF iwe makini na hili," alisema Mayanja.
Katika mchezo huo Kagera ilijikuta ikiruhusu mabao 2-0 mbele ya wapiga debe hao ambao wamekuwa kwenye kiwango cha juu tangu walipofanyiwa programu na mshambuliaji mahiri wa zamani wa Barcelona na timu ya taifa ya Uholanzi Patrick Kluivert.
Kocha Jackson Mayanja akishangilia kwenye moja ya mechi za timu yake