Katika moja kati ya
hotuba zake Baba wa Taifa mwalimu Julias Kambarage Nyerere aliwahi
kuizungumzia Afrika na kuisikitikia mno Afrika ,anasema alikuwa hajui kama
Afrika ni tegemezi tegemezi tegemezi
kweliiii,tegemezi ki uchumi ,kisiasa na kila kitu,Afrika kila kitu inategemea
kwa Wazungu na mbaya zaidi hata mawazo yao yanatoka kwa Wazungu alisema ni
tegemezi tegemezi tegemezi saaana,aliwaona wale Mazungu Karne ijayo yatakuwa
mbali mno na sisi ,na sisi tutaendelea
kuwa kama Madodoki ni kupokea tu iwe uchafu au usafi,alifika mbali ,mno na
kusema kuwa Afrika itakuwa kama Mbuga kubwa mno wazungu watakuwa wanakuja kama
watalii tu kwetu.
Wiki iliyopita timu ya Stand United ilimtimua kocha wake
Emanuel Masawe kwa kile uongozi walichodai kuwa anawagawa wachezaji, na kuwa
ndio chanzo cha timu hiyo kufanya vibaya,kwangu mimi sikushangaa na kauli hiyo
kwani ni ya kawaida mno kwa viongozi wetu wa soka punde wanapowatimua makocha
wao.
Kilichonivutia zaidi kwa kocha Masawe ni siku moja baadaye
kufunguka na kusema kile kilichomuondoa na ambacho makocha wengi simaanishi
wazalendo ni wale wanaofundisha soka Tanzania bila kujali wametoka Zambia ,Serbia
au kwingineko wamekuwa tegemezi tegemzi tegemezi kweli katika hilo,Masawe
alikataa kupangiwa list na viongozi na mbaya zaidi hata mazoezini
hawaonekani,safi sana Kocha Masawe safi mnoooo.
Makocha wengi wanaofundisha soka Tanzania wanawaogopa
viongozi wanaowalipa vi mishahara vya kawaida mno kwa kuwa tu hawana shughuri
nyingine yeyote ya kuwaongezea kipato zaidi ya soka leo wamejikuta wakiwa
tegemezi kwa kila kitu kuanzia kufundisha hadi kupanga timu wamekosa kabisa
meno kulingana na taaluma yao,Masawe leo kanikumbusha jinsi makocha
tunavyotakiwa tuwe ni vyema asubuhi tukauza Nyanya jioni tukaenda kufundisha
Mpira.
Takriban miaka minne iliyopita nilikuwa katika kipindi
kimoja cha TV na wadau wengi wa soka ,baadhi ya waliokuwepo kwa sasa ni
viongozi wakubwa kabisa ndani ya club ya Simba(Kaburu,Tully),viongozi wale
ambao kwa wakati ule mmoja alikuwa simba na mwingine Ashant ,mmojawapo alisema
Tanzania hakuna Makocha ,sisi kocha wetu Patrick Phill tunampangia sisi list ya
kucheza,nilisimama kuipinga mno hoja hiyo kama kocha na bahati mbaya
nimefundisha timu nyingi za mjini Dar kuanzia Ashant,Villa Squad,Vijana
Ilala,Moro United,Yanga Afrikan,Bandari Dar na Mtwara kasoro simbakote huko
kama kuna kiongozi aliyesubutu kuniingilia kwenye list nadhani alikutana na
makali yangu ,Muhsin Baraboo pale vijana,Msafiri Mgoyo pale Ashant,Kifukwe na
Malinzi pale Yanga,Godigodi pale Villa na Ismail Aden Rage pale Moro hao wote
wananitambua sikuwahi kuwa tegemezi kwa kuwa mimi nauza kwanza nyanya soka
baadaye.
Makocha ambao tulidhani ndio ngozi nyeupe au wanatoka nje labda wataheshimu taaluma yao ndio hao
wanapangiwa list,leo timu inacheza Zanzibar katika maandalizi yote ya kombe la
mapinduzi mchezaji hayupo ,yupo kwao tena mapumzikoni anarudi kocha Mzungu
anampanga kesho kama hajapangwa na viongozi atakuwa amepangwa na nani!!!!!!
Safi sana masawe.
Wapo makocha wamekuwa na misimamo hadi unasikia raha ndugu
yangu Sebastian Nkoma ni kocha maskini kabisa lakini kila siku misimamo yake
inamfanya viongozi wamwone hafai na yeye kwa ku heshimu taaluma anamwaga
vumbi,Eugen Mwasamaki pamoja na umaskini akiwa timu ya Tesema leo inamilikiwa
na Halmashauri ya Kinondoni hakukubali
kuyumbishwa na watu wanaojiita wa mpira wakati ni madiwani tu na wengine
hawajui kabisa mpira zaidi za kuwa Wahasibu tu wa Halmashauri ,alipoambiwa
aondoke saa 3 asubuhi yeye saa 12 alfajiri alikuwa tayari kafungasha virago
karudi Karume kufundisha timu za watoto bureeee kabisaa,Mbeya City tumeshuhudia
kocha Juma Mwambusi akiwaumbua mashabiki na viongozi wake kuwa
maisha yake yote ataheshimu taaluma akabwaga manyanga wenyewe wakamrudisha
,Tanzania tumebaki na makocha wachache mno wa aina hiyo wengi wamekuwa ni
mizigo ,na akili zao zimeshikiwa na viongozi na mbaya zaidi viongozi hao ndio
wanaopita kwa mashabiki na kuwaambia kesho tutamwambia mwalimu apange list ya
wazawa watupu hao wageni tupa nje na kweli kesho unakuta listi ya wazawa watupu
mbele unamwona Javu unamwona Tegete ndio makocha wetu.
Makocha wanaofundisha Tanzania bila kujali wanatoka nchi
gani ,kama atakaa zaidi ya miezi sita nchini huyo sio kocha lazima atapangiwa
listi,Trot Moloto moja kati ya makocha bora Afrika kusini alipoambiwa neno moja
tu panga list hii yeye aligongo viza yake kurudi kwao na hajaonekana tena huyo
ndio mfano wa kocha.
Makocha mnaofundisha soka Tanzania mtaendelea kuwa tegemezi
tegemezi hadi lini,ukocha ni taaluma ingawa kila mtu anajifanya anajua ukocha
ndio maana leo nawapa bravo Juma Mwambusi mbeya city na Emanuel Masawe Stand
United.
Mwandishi wa makala hii ni mfanyakazi wa Mamlaka ya
usimamizi Bandari anapatina Kennedymwaisabula@gmail.com
06528757YANGA MALIZENI MECHI TAIFA NA SI VINGEVYO.
Mwaka 1973 nikiwa darasa la kwanza Simba Sports Club ikiwa
ndani ya uwanja wa Taifa katika mechi yake ya Club Bingwa ya Afrika ngazi ya
nusu fainal ilikutana na timu toka Misri inaitwa Mehal El Cubra ,hadi
mwisho wa mpambano huo ambao sisi tuliokuwa watoto tulikuwa tuna njia nyingi
mno za kuingia uwanjani sijui siku hizi watoto wa leo wana njia zipi ,lakini
sisi tulikuwa tunaweza kuwahi kufunga nyavu na kupachika Vibendera,kuruka ukuta
ambao kwa wakati ule ulikuwa ni mrefu sana kulingana na vimo vyetu lakini
tutafanyaje,au nimshike mkono mtu yeyote mzima niingie naye,achilia ile ya
kukaa juu ya miti na kusubiri dakika 10 za mwisho fungulia Mbwa,Simba ilikuwa
imeibuka na ushindi wa goli moja kwa bila goli lililofungwa na Saady Ally
nalikukmbuka hadi leo miaka zaidi ya 40 imepita.
Watanzania wengi walijua kuwa kuwa Simba imemamaliza mchezo
tayari na ukizingatia mziki uliokuwepo wakati ule ukiongozwa na Athuman Mambosasa
golini wengine Shaban Baraza,Mohamedy Kajole,Omary Chogo,Haidar Abeid,Halid
Abeid ,Willy Mwaijibe,Adam Sabu ,Abdalh Kibadeni, na wengineo wengi tu ni kwa
nini tufungwe!!!!!! Kumbe wapi tukaonewa tukapigwa tukazomewa na mwisho wa siku
tulipigwa goli moja na katika eneo la penalt tano tano Marehemu Mambosasa
angekuwepo angesimulia tukayaaga mashindano fainal tukaikosa hatukujua mbinu za
kumaliza mchezo.
Mwaka 1985 nikiwa nacheza timu ya soka ya Mwadui tulipata
bahati ya timu nzima kwenda na gari letu mjini Mwanza chini ya kiongozi wetu
Chief Kihiyo kwenda kushuhudia pambano la club bingwa ya Afrika kati Simba na
National El Ahaly ya Misri,niliishuhudia
timu hiyo ya Misri ikitumia dakika 10 tukamaliza mchezo baada ya kupiga basi
karibia 30 hivi na kumpelekea mfungaji wao bora kabisa wakati huo tena Barani
Afrika Mohamud El Hatibu maarufu kama Bibo ambaye alimshambua kiraini kabisa
kipa Mozes Mkandawile,ingawa matokeo ya mechi ile hadi mwisho Simba iliibuka na
ushindi wa magoli 2-1 magoli yaliyofungwa na Zamoyoni Mogela na Mtemi Ramadhani
lakini wa Misri wale walishamaliza mchezo dakika 10 tu za
mwanzo wenzetu wanaojua soka ndicho kitu walichotuzidi kujua kumaliza mchezo.
Mnamo miaka ya 80 katikati Yanga walikumbana tena na timu
toka Misri na mechi ya awali walianza Misri ,yanga ikijengwa na ukuta wa Berlin
uliongozwa na Athuman Juma Chama,Yusuph Bana,Ahmedy Amasha ,Allan Shomari
wenyewe wakimwita Moringe,Juma Mkambi ,Fred Minziro golini akiwa Juma Mhina
,pamoja na ugumu wa ukuta huo iliwachukua dakika 10 za mwisho baada ya
kumchosha mno Amasha na kuandika goli 5 na baada ya dakika 90 ubao ulisomeka
5-1 mechi wakawa wameshaimaliza hapa wakaja kutalii tu na kutoka sare 1-1 na
bahati kocha msaidizi wa Yanga leo Charles Boniface Mkwasa alikuwepo katika
mechi hiyo na goli moja alifunga yeye.
Yanga wiki hii
inakumbana na timu kutoka Zimbabwe inaitwa Platinum ni lazima imalize mchezo
Dar es saalam na si sehemu nyingine yeyote,wawakilishi wenzao Azam Walishindwa
kumaliza mchezo pale Chamazi matokeo yake ndio hayo tuliyoyasikia,ili umalize
mchezo ni lazima kila nafasi inayopatikana watu washangilie bao,ni lazima tuwe na hazina kubwa ya mabao
nyumbani,kwa wenzetu wanaojua kumaliza mchezo watakuja wakiwa wameficha makucha
yao huenda hata washambuliaji wao muhumu kama vile sisi Msuva na Ngasa huenda wakakaa jukwaani
wanatusoma tu ili waje wamalize mchezo kwao.
Kocha Mdachi Hans Pluijm na bench lake la ufundi ni lazima wafundishe wachezaji faida ya
kutumia kila nafasi wanayoipata kwa kuweka mpira kambani kinyume cha hapo
tutatafuta sababu nyingi mno katika mechi ya marudiano pale Harare wiki mbili
baadaye,ni lazima timu iwe na hazina ya magoli yasiyopungua manne kinyume na
hapo mchezo tutakuwa hatujaumaliza dar na mchezo unatakiwa umalizwe katika
uwanja mkuu wa Taifa siku ya terehe 14 March.
Timu nyingi za kwetu kuanzia wachezaji ,viongozi na
mashabiki hatujui sehemu ya kumalizia mashindano ndio maana usiku ule katika
uwanja wa Chamazi kwenye mechi ya Azam na El Merreck ya Sudan wakati wachezaji
,viongozi na mashabiki wakati wakishangilia ushindi ule wa magoli mawili wenye
kuangalia kwa jicho la tatu muda huo huo tukasema mchezo huu bado haujaisha
utakwenda kwisha Sudan,Yanga tunatakiwa tuwe na mshikamano mkubwa ushindi
wowote wa goli chache tujue mchezo haujaisha!!!!!
kennedymwaisabula@gmail.com