Azam timu inayomilikiwa na mfanyabiashara maarufu hapa nchini Said Barhessa ,wiki iliyopita ilijikuta ikitolewa tena katika michuano ya Afrika na timu ngumu mno ya El Merreikh ya Sudan kwa jumla ya magoli 3-2.
Baada ya mchezo wa mwisho uliochezwa Nchini Sudani viongozi wa Azam walikuja na malalamiko kibao,walinukuliwa wakidai kuwa Waamuzi hawakuwa sahihi katika maamuzi yao,kiasi kwamba waliwatoa mchezoni wachezaji wetu,na kwamba muda wote waamuzi walikuwa wako makini mno katika matukio yetu kuliko yao, na njama nyingi za nje ya uwanja ziliashiria kuwa ni lazima tupoteze mechi na kweli hivyo ndivyo ilivyokuwa.
Kwa wadau tuliowazoea Waarabu ni watu wa fitna mno kwa kila kitu na hiyo hatukuwa na mashaka nayo ,lakini kwa mstuko wa wengi tukasikia Menenjment ya timu imekutana na imemtimua kocha wao Joseph Omog Raia wa Cameroon pamoja na msaidizi wake Ibrahim Shikanda,
Tunajiuliza kama viongozi walioambatana na timu wamekiri kuwa timu ilihujumiwa sasa kocha anaingiaje katika lawama hadi kutimuliwaaaa
AZAM WALIA NA MWAMUZI LAKINI KOCHA OUT
Info Post