Breaking News
Loading...
Wednesday, 4 March 2015

Info Post
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), huenda likamchukulia hatua za kinidhamu Ofisa Habari wa Yanga Jerry Muro kwa kile kinachoelezwa kuwa amekua akitoa kauli za kichochezi zinazoweza kuhatarisha usalama na kuleta vurugu.
Taarifa za ndani kutoka shirikisho hilo, zinasema kuwa Muro ataadhibiwa kwa kuzingatia kanuni ya TFF inayokataza shabiki, mchezaji au kiongozi kutoa kauli inayoweza kuhamasisha vurugu, fujo au uvunjifu wa amani.
"Huyu Bwana tumemvumilia sana na uvumilivu wetu utafikia kikomo muda si mrefu. Ipo kanuni inayoipa nguvu kamati ya nidhamu na maadili ya TFF kumfungia yeyote anayetoa kauli za kichochezi. Sasa kwa kuwa yeye bado anaendelea kutoa kauli za kuchochea watu dhidi ya TFF, sheria itafuata mkondo wake," alisema mtoa habari huyo ambaye hakupenda jina lake liwekwe hadharani.
Miongoni mwa kauli ambazo zinaweza kumuweka Murro matatani, ni ile aliyoitoa jana ambapo alinukuliwa akisema kuwa TFF ijiandae kucheza mechi ya ligi dhidi ya JKT Ruvu, iwapo mechi hiyo itachezwa tarehe 11 mwezi huu.