Breaking News
Loading...
Wednesday, 4 March 2015

Info Post
Yanga imejichimbia huko Bagamoyo kujiandaa na pambano la watani wa jadi dhidi ya Simba Jumapili, huku Kocha wa timu hiyo Hans Pluijm aktamba kufuta uteja wa timu yake dhidi ya Simba.
Akizungumza na Mwandishi wetu jana, Pluijm alisema kuwa falsafa ya timu yake kwa sasa ni kushinda kila mechi ili waweze kutwaa ubingwa na anaamini hilo linawezekana kutokana na uwezo wa kikosi chake kwa sasa.
" Yanga ndiyo timu yenye kikosi bora hapa nchini kwa sasa na pia tunaongoza ligi. Sioni namna Simba wanaweza kuepuka kufungwa Jumapili, kwani tunajiandaa kikamilifu. Nawaomba mashabiki wetu wajitokeze kwa wingi," alisema Pluijm.
Nae nahodha wa timu hiyo Nadir Cannavaro, alisema kuwa mazingira ya kambi yao ya sasa yanawapa hamasa wao wachezaji kufanya vizuri kwenye mchezo wa Jumapili.
Cannavaro alisema kuwa utulivu uliopo kwenye Hoteli ya Kilomo Resort ambayo wapo kambi kwa sasa, yanafanya akili yao itulie na kuwajenga vyema kisaikolojia.