Shirikisho la soka Tanzania (TFF) limeangusha adhabu kwa
baadhi ya timu za Ligi Daraja la Pili baada ya kubaini uvunjaji
wa kanuni uliofanywa na timu hizo.
Tarrifa iliyotolewa jijini leo kupitia kwa msemaji wa TFF
Baraka Kizuguto baadhi ya timu zilizopata adhabu ni Ujenzi
Rukwa na Volcano FC ya Morogoro huku pia baadhi ya
viongozi na wachezaji nao wakiadhibiwa.
Ujezi Rukwa na Volcano zimeshushwa daraja mpaka ligi ya
Wilaya baada ya kushindwa kufika uwanjani kwenye mechi
zao dhidi ya Mvuvumwa na Wenda, Magereza Iringa imetozwa
faini ya Tsh. 200000 baada ya kuchelewa kwenye kikao cha
maandalizi ya mechi, AFC imetozwa Tsh. 300000 baada ya
mashabiki wake kufanya vurugu kwenye mechi dhidi ya
Bulyanhulu wakati viongozi wa Mbao FC Abdallah Chuma
na Yasin Abdul wakifungiwa miezi sita na Faini ya Tsh.
100000 kila mmoja baada ya kumtukana nakumtishia maisha
Kamishina wa mechi dhidi ya AFC
Singida United imepewa pointi tatu dhidi ya Ujenzi Rukwa ambayo ilimchezesha mchezaji asiyestahili.
TFF yaangusha Rungu Daraja la Pili
Info Post