Marehemu Adamu ni moja kati ya makocha waliopata
kunifundisha soka kwa kipindi kirefu ,katika moja ya hadithi zake nyingi
alizokuwa akitusimulia yeye na Mzee Kilambo aliwahi kutusimulia mechi iliyopigwa miaka ya sabini
mwishoni dhidi ya timu yake ya Simba Sports Club na TPC ya Moshi,mechi ambayo
iliishia kwa Simba kushinda goli mbili
kwa bila na yeye Adam Sabu
maarufu kama Gud mullar alitupia yote mawili.
Sabu alituambia wakati ule Simba ilikuwa imemsajili kijana
mmoja ambaye alikulia Morogoro wakati Sabu anacheza mpira karikuwa katoto
kadogo mno,sasa ndio roho ya Simba chochote atakachosema viongozi watakuwa
wanamsikiliza yeye,alikuwa anaitwa Aluu Ally,kwa wale waliopata bahati ya
kumuona watakubaliana nami kuwa Aluu Ally ni moja kati ya viungo bora kabisa
waliopata kutokea katika Nchi yetu.
Wakati mchezo umemalizika Sabu akitoka na furaha ya kufunga
magoli mawili Aluu Ally alitoka analia ,hakupenda kabisa matokeo yale na viongozi wa Simba walipomfuata kumnyamazisha
na kumuuliza kulikoni alijibu Simba ni timu kubwa huwezi kuwa na wachezaji wa
aina ya Adam Sabu nimempa mipira 18 pasi za uhakika anafunga goli mbiliii!!!!
Hafai kuwepo katika timukubwa kama hii,
Sabu alilia saana baada ya kusikia kauli hiyo ya kijana huyo aliyemwacha
Morogoro akiwa Kinda kabisa ndio soka lilivyo.
Haraka sana nikamkumbuka Said Bahanuzi aliyepelekwa kwa
mkopo Polisi ,nimeshuhudia mechi zake karibu tatu alizocheza akiwa na Polisi
moja ikiwa pale Mkwakwani alikosa magoli mengi mno, mechi nyingine ni ya juzi
tu tuliyoiona kupitia Azam Tv dhidi ya Kagera Sugar pale Kambarage Shinyanga
ambapo walifungwa goli moja kwa bila nay eye
Bahanuzi akiwa amepoteza baadhi ya nafasi za wazi mno ,niliwauliza
viongozi wake baada ya mchezo kwisha wakaniambia leo bhana afadhali Mtwara dhidi ya
Ndanda alikosa karibu Kumi za wazi,vijana akina Bantu Admin,Mgangai kazi yao
wenyewe ni kumpelekea tu Bahanuzi ashindwe na timu haina mashabiki akikosa
wanarudi kati kukaba.
Ni lazima nikiri kuwa miongoni mwa watu walioshiriki
kumpeleka Yanga kwa njia moja au nyingine alikuwa ni mwandishi wa makala hii na
kweli aliingia na kufanya vizuri mno katika michuano ya Kagame na kuibuka kuwa
mfungaji bora,basin a soka lake akaliacha katika michuano hiyo,kukawa na
hadithi nyingi zinazomuhusu yeye za nje ya uwanja,Maskini Bahanuzi hakupata mtu
wa Saikoloji jiji akaliingia kwa pupa soka likamshinda,pamoja na kuitwa timu ya
Taifa bado kocha aliona bado anahitaji marekebisho makubwa kwake ili awe
mchezaji wa timu kubwa.
Wiki iliyopita nilistushwa kusikia Said Bahanuzi amekuwa
mchezaji bora wa mwezi,naweheshimu wataalamu hao wanaochagua wachezaji bora wa
mechi lakini sikuelewa kama kweli wana vigezo gani muhimu kumpitisha mchezaji
huyo ambaye kwangu me naona amewanyima nafasi nyingi mno Polisi za kuibuka na
ushindi na naamini hata kama angeulizwa Kocha Adolf Richard asingemtaja
Bahanuzi.
Bahanuzi soka lake sasa limehamia mdomoni kila kukicha
anaeleza habari za kishirikina tu na anasahau soka na mambo hayo ni kiini macho
tu na ninavyomfahamu Said ni mtu wa Ibada mno ni vipi aweke imani kubwa mno
katika mambo ya giza, ndio maana Mbwana Samata,Thomas Ulimwengu wasoka nje ya
nchi kwa juhudi za mazoezi tu,ni kawaida ya wachezaji wengi mno wanaofikia umri
mkubwa wanaanza kuongea na mpira unahamia mdomoni zaidi kuliko kwenye miguu.
Kwa Bahanuzi umri wake bado ni mdogo hivyo ana kila sababu
ya kusahau mambo ya timu kubwa kama Simba na Yanga zenye washabiki wengi wenye
uwezo mkubwa wa kusoma timu zao na hawakosekani katika viwanja ,lakini mbaya
zaidi hawana subira na mtu wa aina ya Bahanuzi anayepata nafasi 18 na kufunga
goli moja hapo ndipo nilipomkumbuka kocha wangu Adamu Sabu.
Bahanuzi acha kuongea piga soka watu wataona lakini kwa
kiwango chako cha sasa mmmm bado me Napata shaka maana soka linachezwa uwanjani
sio chumbani wote tunaliona,na tayari umetoa masharti yanga wakitaka urudi
wakuhakikishie nafasi ya kucheza kwa maana hiyo ,Msuva,Nyonzima ,Tambwe,Ngasa
na Contihon watupwe nje uwepo ndio hapo nachoka kabisaa
Mwandishi wa makala hii anapatikana Email
kennedymwaisabula@gmail.com