Kuzidiwa
katika safu ya kiungo sambamba na benchi la ufundi kushindwa kusoma mchezo kwa
umakini, vimetajwa kuwa sababu kubwa iliyopelekea Yanga kukubali kichapo cha
bao 1-0 jana mbele ya Simba.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti na mwandishi wetu, baadhi ya makocha wa soka nchini
wamesema kuwa safu ya kiungo ya Yanga ilishindwa kuwamudu viungo wa Simba ambao
walitawala vilivyo kwenye mechi hiyo.
“Pluijm
alianza na viungo wawili wakati Simba walikuwa na viungo wengi ambao wanajua
kumiliki mpira. Pia benchi la ufundi la Yanga nadahni lilishindwa kusoma na
kuuelewa kwa haraka mchezo, “ alisema Eugene Mwasamaki.
Nae Kocha
Msaidizi wa Stand United Athumani Bilali, alisema kuwa Simba walicheza kitimu
hasa safu yao ya kiungo wakati Yanga waliingia wakitegemea uwezo wa mchezaji
mmoja mmoja.
Ushindi
dhidi ya Yanga umewapeleka Simba mpaka nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi
wakiwa na 26 huku Yanga wakiendelea kuongoza wakiwa na pointi 31
Wachezaji wa Simba wakishangilia bao la Okwi