Breaking News
Loading...
Thursday, 12 March 2015

Info Post
Yanga imeendelea kumvalia njuga mshambuliaji Ibrahim Ajibu wa Simba, baada ya kupanga kukata rufaa, kupinga kitendo cha Simba kumtumia mshambuliaji huyo huku akiwa na kadi tatu.
Tamko hilo la Yanga, limekuja huku wakiwa na machungu ya kupewa kichapo cha bao 1-0 na Simba, katika mchezo uliozikutanisha timu hizo Jumapili iliyopita kwa bao la Mganda Emmanuel Okwi.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini jana, Katibu Mkuu wa Yanga Dk. Jonas Tiboroha, alisema kuwa kitendo cha Simba kumtumia Ajibu ni ukiukwaji wa wazi wa kanuni za soka jambo ambalo wao Yanga hawawezi kulifumbia macho mpaka kieleweke.
"Simba walimtumia Ajibu kwenye mechi dhidi yetu, huku wakijua kabisa kuwa na kadi nne za njano. Kanuni za soka ziko wazi na kila mmoja analifahamu. Sisi hatutokubali na tutakata rufaa kulipinga jambo hilo," alisema Dk. Tiboroha.
Hata hivyo huenda rufaa ya Yanga ikatupiliwa mbali na TFF kwani tayari Kamati ya Utendaji iliketi na kupitisha kanuni inayoruhusu mchezaji kuchagua mechi ya kucheza pindi anapokuwa na kadi tatu za njano.