Beki wa kati Matts Hummels anayechezea Borussia
Dortmund, amesema kuwa ataamua hatma yake ndani ya
klabu hiyo ndani ya kipindi cha wiki chache zijazo.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26, mkataba wake ndani
ya timu hiyo ya Dortmund umebakiza kipindi cha miaka miwili
lakini kumekuwa na hofu ya mlinzi huyo wa Kimataifa wa
Ujerumani kutimka mwishoni mwa msimu huu ikiwa timu hiyo
haitafanikiwa kupata nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa
msimu ujao.
Inadaiwa kuwa Manchester United ni miongoni mwa timu
ambazo zimekuwa zikiisaka kwa udi na uvumba saini ya
Hummers, ikitajwa kuwa wametenga kiasi cha Pauni milioni 35
ili kumnasa beki huyo.
Hata hivyo Hummers amekanusha kuwa anaangalia kama
Dortmund itaingia kwenye Ligi ya Mabingwa kama wengi
wanavyovumisha na amepanga kupeleka maoni yake kwa
uongozi wa timu hiyo juu ya usajili kwa ajili ya msimu ujao.
"Siwezi kukubaliana na hali kama hiyo kwa namna moja au
nyingine. Ninaongozwa na akili yangu kufanya maamuzi.
Mambo yatakuwa wazi baada ya wiki chache," alisema
Hummers.
Kauli ya Hummers huenda ikaongeza presha kwa Dortmund
ambayo ipo kwenye nafasi ya kumi katika msimamo wa Ligi
Kuu nchini Ujerumani maarufu kama 'Bundesliga'
Hummers aiweka njiapanda Dortmund
Info Post